Bunge la Afrika Kusini limesema, litajadili daftari la utaratibu kuhusu kumwondoa rais Jacob Zuma madarakani.
Mwishoni mwa mwaka jana mahakama ya kikatiba ilitoa hukumu kuwa bunge lilishindwa kuweka kanuni mwafaka za kumwajibisha Rais Jacob Zuma na kashfa ya Nkandla, ambapo Rais Zuma alituhumiwa kutumia vibaya fedha za umma zipatazo dola za kimarekani milioni 20 kwa ajili ya kuimarisha usalama nyumbani kwake Nkandla, katika jimbo la KwaZulu-Natal.
Mahakama hiyo ililitaka bunge la Afrika Kusini litunge kanuni bila kuchelewa ili kuanzisha utaratibu kwa mujibu wa kifungu cha 89 cha katiba.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |