• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Coutinho afurahia kutua Barcelona

    (GMT+08:00) 2018-01-08 09:34:37
    Hatimaye ndoto ya nyota Philipe Coutinho wa Brazil ya kucheza Barcelona imetimia baada ya klabu yake ya Liverpool kukubali kumuuza kwa dau la pauni milioni 146.

    Kufuatia taarifa hiyo, Coutinho mwenyewe ameeleza kufurahia tukio hilo wakati wa mahojiano na televisheni ya Barcelona.

    Mchezaji huyo anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya leo kabla ya kukamilisha tukio la kusaini rasmi mkataba.

    Nyota huyo mwenye miaka 25, huenda akacheza kwenye mechi ya Copa Del Ray itakayopigwa alhamisi dhidi ya Celta Vigo katika dimba la Nou Camp.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako