• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kombe la FA: Arsenal wavuliwa ubingwa rasmi na Nottingham Forest

  (GMT+08:00) 2018-01-08 09:34:59
  Mabingwa watetezi wa kombe la FA nchini Uingereza Arsenal, jana wamevuliwa ubingwa huo na Nottingham Forest kwa kufungwa magoli 4-2.

  Hii ni mara ya kwanza kwa Arsenal kuondolewa katika raundi ya tatu ya michuano hiyo tangu mwaka 1996 walipoondolewa na Shiefield United.

  Magoli ya Nottingham Forest wanaoshiriki ligi daraja la kwanza, yamefungwa na Eric lichaj aliyefunga mawili dakika ya 20 na 44, Ben Brereton akifunga la tatu kwa njia ya penati na goli la nne likifungwa na Kieran Dowell kwa njia ya penati pia.

  Magoli ya Arsenal ya kufutia machozi yalipatikana kupitia Per Metsacker na Danny Welbeck.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako