• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wahamiaji karibu 300 waokolewa katika pwani ya Libya

    (GMT+08:00) 2018-01-08 09:54:26

    Msemaji wa jeshi la majini la Libya Bw. Ayob Qassem, amesema jeshi hilo limewaokoa wahamiaji haramu 297 na kupata miili miwili kwenye eneo la bahari lililoko karibu na pwani ya mji wa Garrabulli, kilomita 60 mashariki mwa Tripoli.

    Msemaji huyo ameongeza kuwa miili miwili ni ya wanawake, mmoja wao alikuwa mjamzito, na kwamba vifo vyao vinatokana na boti walizokuwa wakisafiria kujaa wahamiaji kupita kiasi.

    Libya imekuwa nchi inayotumiwa na wahamiaji haramu kuvuka bahari ya Mediterranean kwenda Ulaya, kutokana na kukosekana kwa usalama nchini humo, baada ya kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Muammar Gaddafi kuondolewa madarakani mwaka 2011.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako