• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika waahidi kuimarisha mafunzo kwa polisi wa Somalia

    (GMT+08:00) 2018-01-08 09:54:56

    Tume maalumu wa Umoja wa Afrika ya kulinda amani nchini Somalia (AMISOM) imesema itaimarisha mafunzo kwa vikosi vya usalama wa Somalia (SPF) ili kuviwezesha kuchukua majukumu zaidi ya kulinda usalama nchini humo.

    Naibu mwakilishi maalum wa mwenyekiti wa Umoja wa Afrika nchini Somalia Bw. Simon Mulongo amesema mpango huo unalenga kuvijengea uwezo vikosi vya SPF hadi kufikia kiwango cha kukubalika kimataifa.

    Vikosi vya AMISOM vinatarajiwa kukabidhi majukumu ya kulinda usalama wa miji muhimu kwa vikosi vya Somalia kutokana na mpango wa mpito unaozingatia hali halisi. Na chini ya mkakati wa kuondoka, askari elfu moja wameondoka Somalia kabla ya mwisho wa mwaka jana, na badala yake AMISOM itapeleka maofisa 500 wa polisi nchini humo ili kuimarisha mafunzo kwa polisi wa Somalia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako