• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yapata matokeo ya uvumbuzi katika sekta nyingi za sayansi na teknolojia

  (GMT+08:00) 2018-01-08 17:30:46

  Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC na baraza la serikali ya China leo imefanya mkutano wa kutoa tuzo za mwaka 2017 za sayansi na teknolojia, ambazo zimetolewa kwa miradi 271 na wanasayansi 9, pamoja na wageni 7 waliopata tuzo ya ushirikiano wa kimataifa katika shughuli za sayansi na teknolojia.

  Rais Xi Jinping na viongozi wengine wa China wametoa hati za tuzo kwa watu waliotuzwa. Waziri mkuu Li Keqiang amehutubia mkutano huo kwa niaba ya kamati kuu ya CPC na baraza la mawaziri, akisema tangu mkutano mkuu wa 18 wa CPC, China imepata mafanikio makubwa katika shughuli za sayansi na teknolojia, ambayo yametoa mchango muhimu kwa ajili ya maendeleo ya uchumi na jamii nchini China.

  Katika majira ya mchipuko mwaka 2013, homa ya mafua ya ndege aina H7N9 ilitokea ghafla katika sehemu ya pembetatu za mto Yangtze, hali ambayo ilifuatiliwa na jumuiya ya kimataifa. Ili kukabiliana na maradhi hayo, chini ya uongozi wa mwanataaluma wa Akademia ya Uhandisi ya China Bi Li Lanjuan, hospitali ya kwanza ya taasisi ya udaktari ya Chuo Kikuu cha Zhejiang ilianzisha jukwaa la ngazi ya kitaifa, na kupata mafanikio makubwa katika kugundua na kuthibitisha chanzo kipya cha virusi, kudhihirisha utaratibu wa ugonjwa, matibabu, na kutengeneza chanjo mpya. Mafanikio hayo yamepata tuzo ya ngazi ya juu zaidi ya maendeleo ya sayansi na teknolojia ya mwaka 2017. Kwani hii ni mara ya kwanza ya China kukabiliana na maradhi mapya ya kuambukiza yaliyotokea nchini kwa njia ya kichina. Baadaye njia hiyo pia ilitumiwa katika kupambana na maradhi ya Ebola kwa mafanikio. Bi Li anasema,

  "Tuna maabara ya kisasa ya P3 na kikundi hodari cha kuchunguza virusi. Hadi sasa tunaendelea na kazi ya kuchunguza virusi vinavyobadilika. Tumejenga mtandao kamili, kama virusi vipya vikitokea, tunaweza kuvipima mara moja."

  Licha ya miradi mikubwa inayolingana na mkakati wa taifa, tuzo hiyo pia imetolewa kwa uvumbuzi unaolengea kuboresha maisha ya watu. Katika miaka ya hivi karibuni, uchafuzi wa hewa unafuatiliwa zaidi na watu. Kwa mujibu wa matokeo yaliyopatikana ya utafiti, matumizi ya makaa ya mawe ni chanzo kikuu cha uchafuzi huo. Mradi wa "teknolojia ya kupunguza kabisa utoaji wa uchafuzi wa vinu vinavyotumia makaa ya mawe" umepata tuzo ya ngazi ya kwanza ya uvumbuzi wa teknolojia. Kiongozi wa mradi huo Bw. Gao Xiang amesema, kabla ya hapo, wameendelea na utafiti kwa miaka zaidi ya 10. Hivi sasa teknolojia hiyo inatumiwa katika vinu zaidi ya 300 vya viwanda vya kuzalisha umeme kwa makaa ya mawe. Anasema,

  "Teknolojia yetu inaweza kupunguza Sulfur dioxide kwa asilimia 83, Nitrogen oxides kwa asilimia zaidi ya 50, na vumbi asilimia 67. Baadaye viwanda vya kuzalisha umeme kwa kuwasha makaa ya mawe havitachukuliwa kama chanzo cha uchafuzi."

  Katika miaka ya hivi karibuni, China imetilia maanani utafiti wa sayansi ya kimsingi, na kupiga hatua kubwa. Mara hii, tuzo ya ngazi ya kwanza ya sayansi ya asili imetolewa kwa mradi wa AIE. Kiongozi wa mradi huo Bw. Tang Benzhong anasema,

  "Tunaweza kuchukulia AIE kama ni kigunduzi cha kutafuta chembehai za saratani. Ina uwezo wa kwenda sehemu zenye chembeihai nyingi za saratani mwilini mwa binadamu, na kutoa ishara kwa madaktari."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako