• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda yakanusha kufanya makubaliano na Isreal kuhusu wahamiaji

    (GMT+08:00) 2018-01-08 18:54:05
    Serikali ya Uganda imekanusha taarifa kuwa imefikia makubaliano na Israel ya kuwahifadhi maelfu ya waafrika wanaotafuta hifadhi walioamriwa kuondoka nchini katika taifa hilo la Mashariki ya Kati ndani ya kipindi cha miezi mitatu ijayo au kufungwa jela.

    Waziri wa mambo ya kimataifa wa Uganda, Henry Oryem Okello aliliambia shirika la habari la Xinhua kwamba, hakuna makubaliano yaliyoingiwa kati ya taifa hilo la Afrika Mashariki na Isreal ili kuwapa hifadhi watu 35,000, wengi wao wakiwa ni kutoka Eritrea na Sudan.

    Katika maneno yake kiongozi huyo pia amesema, hata wao hawajui habari hizo imetokea wapi, na wala taifa lake halijaingia makubaliano yoyote ya kurejesha wakimbizi nchini Uganda.

    Wiki iliyopita mamlaka za Israel ziliwapa muda wa siku 90 raia wa nchi za Afrika walioingia katika taifa hilo kutafuta hifadhi kutokana na sababu za kivita na mateso, wawe wameondoka kurejea kwenye nchi zao au kwenye nchini nyingine mbadala, au la watakabiliwa na kifungo jela.

    Mamlaka inayohusika na idadi ya watu pamoja na masuala ya uhamiaji ya Israel imesema kuwa, wale wote watakaoondoka kabla ya mwezi Aprili watapewa pesa yenye thamani ya dola za kimarekani 3,500, nauli ya ndege pamoja na marupurupu mengine ya uhamisho.

    Kwa mujibu wa Ripoti, Wahamiaji kutoka Afrika wamepewa nafasi ya kuchagua kurejea kwenye nchi zao, au kupelekwa Uganda au Rwanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako