• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wa Zambia waapa kumtii rais wa nchi hiyo

    (GMT+08:00) 2018-01-09 09:01:03
    Mawaziri wa Zambia wameapa kumtii Rais Edgar Lungu wa nchi hiyo, na kuahidi kuwa watakuwa naye bega kwa bega.

    Waziri wa habari na utangazaji Bibi Kampamba Mulenga amesema, kinyume cha ripoti zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba baraza la mawaziri la nchi hiyo limekuwa likiporomoka, mawaziri wa nchi hiyo wameahidi kuendelea kuwa watiifu na kushikamana na rais.

    Wiki iliyopita waziri wa mambo ya nje Bw. Harry Kalaba alijiuzulu akieleza kushindwa kwa serikali kupambana na ufisadi, hali ambayo imeleta wasiwasi kuwa mawaziri wengi zaidi wanatarajiwa kujiuzulu.

    Bibi Mulenga amesema baada ya mkutano wa baraza la mawaziri, mawaziri wameonesha utiifu na imani yao kwa utawala wake.

    Rais Lungu Jumatatu alimteua mbunge wa chama tawala PF Bw. Joe Malanji, kuwa waziri mpya wa mambo ya nje, na mbunge mwingine wa chama hicho Bw. Alexander Chiteme aliteuliwa kuwa Waziri wa mpya wa mipango ya maendeleo, ili kuchukua nafasi ya Lucky Mulusa aliyefukuzwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako