• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Operesheni za kijeshi dhidi ya Kundi la IS nchini Iraq zasababisha watu 700 kupoteza makazi

    (GMT+08:00) 2018-01-09 09:18:29

    Msemaji wa Umoja wa Mataifa Bw Stephane Dujarric amesema takriban watu 700 wamepoteza makazi yao kutokana na operesheni za kijeshi dhidi ya waasi wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Kundi la IS zilizofanyika mjini Kirkuk, Iraq tangu Alhamisi iliyopita.

    Msemaji huyo amesema Ofisi ya uratibu wa misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa OCHA imeripoti kuwa watu hao waliokimbia mapambano kwenye eneo la Hawija wanahamishiwa kambi ya wakimbizi iliyoko karibu na Daquq, ambako watapewa msaada wa kibinadamu.

    Msemaji huyo pia ameongeza kuwa utoaji wa misaada ya kibinadamu katika eneo la Hawija umesimamishwa kutokana na sababu za usalama, na utarejeshwa mara baada ya operesheni ya kijeshi kukamilika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako