• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lapongeza uchaguzi wa amani Liberia

    (GMT+08:00) 2018-01-09 09:20:07

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepongeza uchaguzi wa Rais uliofanyika kwa amani nchini Liberia.

    Baraza hilo limetoa taarifa ikisema Baraza la Usalama limewapongeza watu wa Liberia na serikali, na viongozi wa kisiasa, mashirika ya kijamii na vyombo vya habari kwa uchaguzi wa amani uliofanyika Desemba 26. Pia limewapongeza wagombea wawili kwa kufanya kampeni zao katika hali ya kuwajibika.

    Taarifa hiyo pia imesema, wajumbe wa baraza hilo wamesisitiza umuhimu wa makabidhiano ya kwanza ya madaraka yenye amani kati ya viongozi waliochaguliwa kwa njia ya kidemokrasia nchini Liberia katika miaka 70 iliyopita. Pia wamesisitiza umuhimu wa mpito wa kisiasa utakaofanyika, na kupongeza ushiriki wa utawala utakaoondoka na utakaoingia madarakani kwenye hafla ya kuapishwa kwa rais mteule Bw George Weah.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako