• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wachambuzi wana imani na sekta ya biashara ya rejareja ya Kenya mwaka 2018

    (GMT+08:00) 2018-01-09 09:20:42

    Kwa mujibu wa wachambuzi, sekta ya biashara ya rejareja nchini Kenya mwaka huu itaendelea kukua vizuri licha ya kuwa baadhi ya wafanyabishara wa rejareja wanakabiliwa na changamoto zinazosababisha baadhi ya maduka kufungwa.

    Shirika la uwekezaji la Cytonn limesema, sekta hiyo itaendelea kuwa na upanuzi wa maduka na kuingia kwa maduka ya kigeni.

    Imefahamika kuwa moja kati ya maduka hayo ya rejareja yanayotaka kupanua biashara kwa mwaka huu ni pamoja na Tuskys, ambayo ni moja ya supamaketi kubwa zaidi nchini Kenya.

    Wiki iliyopita kampuni hiyo ilitangaza mpango wa miaka mitatu kuongeza matawi yake kwa asilimia 56.3 kutoka maduka 64 yaliyopo hivi sasa hadi 100 nchini Kenya na Uganda hadi kufikia mwaka 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako