• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Azarenka ajiondoa kwenye mashindano ya Australia

  (GMT+08:00) 2018-01-09 09:37:10
  Licha ya kupewa nafasi ya heshima ya kushiriki michuano ya tennis ya Australia, bingwa wa zamani wa michuano hiyo, Viktoria Azarenka wa Belarus amejiondoa kwa madai kuwa bado anashughulikia suala la matunzo ya mwanae mwenye miezi 11.

  Nyota huyo mwenye miaka 28 hajashiriki michuano yoyote tangu alipocheza mashindano ya Wimbledon mwaka jana na sasa nafasi yake itazibwa na Ajla Tomljanovic wa Australia.

  Azarenka anaungana na nyota wengine waliojiondoa kwenye michuano hiyo kutokana na sababu mbalimbali akiwemo mwingereza Andy Murray, mmarekani Serena Williams huku Rafael Nadal na Novak Djokivic wakiwa bado hawajulikani hatma zao za ushiriki masindano hayo yanayoanza rasmi Januari 16 mwaka.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako