• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Nottingham Forest yapata kocha mpya

  (GMT+08:00) 2018-01-09 09:37:46
  Klabu ya Nottingham Forest inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Uingereza, imemtangaza Mhispania Aitor Karanka kuwa kocha wake mpya kwa mkataba wa miaka miwili na nusu.

  Kocha huyo aliyeisaidia Middlesbrough kurejea ligi kuu msimu uliopita, anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mark Warburton aliyetimuliwa Disemba 31 mwaka 2017.

  Mechi ya kwanza ya kocha huyo akiiongoza Nottingham itakuwa Janauri 13 timu yake itakapocheza dhidi ya Aston Villa na ikifuatiwa na mechi ya raundi ya nne ya kombe la FA watakapopambana na Hull City.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako