• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Felipe Coutinho atangazwa rasmi kuwa mchezaji wa Barcelona.

  (GMT+08:00) 2018-01-09 09:38:27

  Mchezaji wa kimataifa wa Brazil Felipe Coutinho jana jumatatu amekamilisha zoezi la kuhamia Barcelona ambapo ametangazwa rasmi baada ya kusaini mkataba wa miaka mitano na nusu uliogharimu ada ya pauni milioni 142.

  Kiungo huyo mwenye miaka 25, amekutanishwa na mashabiki waliofurika kwenye uwanja wa Nou ambako alifanikiwa kuzungumzia matarajio yake atakapokuwa klabuni hapo.

  Licha ya kusajiliwa rasmi, Coutinho hataweza kucheza katika kwa kipindi cha takribani wiki tatu kutokana na majeruhi inayomwandama ikiwa na maana kuwa anatarajiwa kurudi uwanjani Februari 4 na mechi yake ya kwanza ikiwa ni dhidi ya watani wa jadi wa Barcelona, timu ya Espanyol.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako