• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika Kusini yaadhimisha miaka 20 ya uhusiano wa kidiplomasia kati yake na China

    (GMT+08:00) 2018-01-09 10:02:36

    Serikali ya Afrika Kusini imeadhimisha miaka 20 ya uhusiano wa kidiplomasia kati yake na China, na kuahidi kutafuta fursa zaidi za kufanya ushirikiano wa kunufaishana kati ya nchi hizo mbili.

    Rais Jacob Zuma amesema ana matumaini ya kuimarishwa kwa uhusiano huo. Idara ya Mahusiano ya Kimataifa na Ushirikiano ya Afrika Kusini DIRCO imetoa taarifa ikisema, katika miaka 20 iliyopita nchi hizo mbili zimefikia makubaliano mengi ya ushirikiano katika sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na biashara, uwekezaji, uchumi na mawasiliano ya umma.

    Afrika Kusini na China zilianzisha uhusiano wa kibalozi Januari 1, mwaka 1998.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako