• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Naibu katibu mkuu wa UM kufanya ziara Syria

    (GMT+08:00) 2018-01-09 10:22:37

    Msemaji wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric amesema, Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya kibinadamu, Bw. Mark Lowcock atafanya ziara yake ya kwanza nchini Syria, ambako anatarajiwa kukutana na wajumbe wa serikali, na kuangalia athari za mapambano nchini humo.

    Bw. Dujarric amesema, katika mwaka wa saba tangu mapambano yaibuke nchini humo, watu zaidi ya milioni 13 wanahitaji msaada wa msingi na ulinzi, na asilimia 69 ya wasyria wanakadiriwa kuishi katika hali ya umaskini mkali, huku mamilioni ya watu wakihitaji ulinzi, chakula, maji safi, makazi na misaada mingine ya dharura.

    Msemaji huyo amesema, katika ziara yake, Bw. Lowcock atakutana na maofisa wa serikali ya Syria, na wajumbe wa mashirika ya kibinadamu, na wadau wengine muhimu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako