• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri wa mambo ya nje wa China kufanya ziara barani Afrika

  (GMT+08:00) 2018-01-09 19:14:55

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang leo hapa Beijing amesema, waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi atafanya ziara nchini Rwanda, Angola, Gabon, Sao Tome and Principe kuanzia tarehe 12 hadi tarehe 16 mwezi huu.

  Bw. Lu Kang amesema, kuimarisha ushirikiano na nchi za Afrika ni msingi muhimu wa sera za diplomasia za China. Katika miaka zaidi 20 iliyopita, ziara ya kwanza ya kila mwaka kwa waziri wa mambo ya nje wa China ni barani Afrika, desturi inayoonyesha kuwa China inazingatia kuendeleza uhusiano kati yake na Afrika.

  Katika ziara hiyo, Bw. Wang Yi atahimiza kutekeleza makubaliano muhimu yaliyofikiwa na rais Xi Jinping wa China na viongozi wa nchi za Afrika, kuimarisha uaminifu wa kisiasa kati ya pande hizo mbili, kuzidisha ushirikiano wa kunufaishana, na kufanya maandalizi kwa ajili ya mkutano wa kilele wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC utakaofanyika nchini China mwaka huu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako