• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yaonya huenda itarekebisha ushirikiano kati yake na IAEA

    (GMT+08:00) 2018-01-09 19:22:07

    Mwenyekiti wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran Bw. Ali Akbar Salehi amesema kama Marekani haitatimiza ahadi ya kutekeleza makubaliano ya suala la nyuklia la Iran kwa pande zote, Iran huenda itarekebisha ushirikiano kati yake na Shirika la Kimataifa la ishati ya Atomiki, IAEA.

    Bw. Salehi amesema hayo alipofanya mazungumzo kwa njia ya simu na Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Yukiya Amano.

    Tarehe 13 Oktoba mwaka jana, Rais Donald Trump wa Marekani alikataa kuidhinisha kwa bunge la Marekani kutekeleza makubaliano ya nyuklia ya Iran.

    Habari zinasema, rais Trump atafanya uamuzi katikati ya mwezi huu kuhusu kama ataweka upya vikwazo dhidi ya Iran.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako