• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Misri na Tanzania kuboresha ushirikiano

    (GMT+08:00) 2018-01-09 19:52:19

    Maofisa waandamizi na wataalamu kutoka sekta mbalimbali wa Tanzania na Misri, wameanza mkutano wa siku mbili wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPC) unaofanyika Misri kujadili mfumo wa kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo.

    Mkutano huo unaandaa misingi ya mkutano wa tatu mawaziri wa JPC utakaohitimishwa kwa kutiliana saini makubaliano mbalimbali katika sekta za kijamii na kiuchumi.

    Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Adolph Mkenda, aliuambia mkutano huo jana kuwa, ushirikiano wa kidugu baina ya Tanzania na Misri uliodumu kwa zaidi ya miongo mitano unahitaji kutiliwa mkazo zaidi katika masuala ya kiuchumi.

    Profesa Mkenda anayeongoza ujumbe wa Watanzania katika mkutano wa wataalamu, alisema inafurahisha kuwa ingawa JPC haijakutana kwa miaka 20 iliyopita, nchi hizi zimeendelea kushirikiana katika nyanja mbalimbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako