• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: PricewaterhouseCoopers yasema ushuru kwa kampuni za bahati na sibu ni wa juu sana

    (GMT+08:00) 2018-01-09 19:52:41

    Shirika la PricewaterhouseCoopers limesema ushuru unaotozwa kampuni za bahati nasibu nchini Kenya ndio za juu zaidi kwenye kanda ya Afrika Mashariki kusini na kati.

    PwC imesema ushuru wa asilimia 35 unaotozwa kwa kampuni hizo na serikali ni ya juu ikilinganishwa na ya Afrika Kusini asilimia 9.6 Rwanda asilimia 13 na Uganda asilimia 20.

    Hivi karibuni serikali ya Kenya ilipandisha ushuru kwa kampuni za bahati na sibu hatua iliopelekea kampuni hizo kuondoa ufadhili wao kwa michezo na pia misaada ya wajibu kwa jamii.

    Nchi zilizoendelea kama vile Ujerumani inatoza asilimia 5 Las Vegas asilimia 6.5 na Canada asilimia 20.

    Afisa wa ushuru kwenye shirika la PwC Steve Okello, amesema ushuru wa asilimia 35 ni mkubwa sana kwa kampuni hizo na huenda ikazilazimi kufunga.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako