• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Mahakama Kenya yaagiza kupakuliwa kwa magunia 800,000

    (GMT+08:00) 2018-01-09 19:53:06

    Mahakama nchini Kenya imeagiza mamlaka ya kukusanya ushuru KRA kuruhusu kupakuliwa kwa magunia 800,000 ya sukari ambayo haikupangiwa kulipiwa ushuru na ambayo imekuwa kwenye bandari ya Mombasa kwa mwezi mmoja.

    Jaji Erick Ogola aliagiza kupakuliwa kwa sukari hiyo ilioko kwenye meli ya MV Iron Lady kutoka Brazil na kuhifadhiwa kwenye bohari la JB Maina.

    Jaji huyo alisema uamuzi uliokuwa umetolwa desemba 27 kuhusu kupakuliwa kwa sukari hiyo ulikuwa sahihi.

    Aidha alikataa kutoa muda zaidi kwa KRA kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

    Mwaka 2016 serikali ilitoa leseni kwa makampuni 60 kuagiza bila ushuru sukari lakini baadaye halmashauri ya sukari ilisimamisha utoaji wa leseni za uagiziaji kutokana na kuwepo kwa kiwango cha juu cha bidhaa hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako