• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Katibu mkuu wa UM akaribisha makubaliano ya kupunguza mvutano kwenye Peninsula ya Korea

  (GMT+08:00) 2018-01-10 08:56:46

  Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amekaribisha makubaliano kati ya Korea Kaskazini na Korea Kusini yanayolenga kupunguza mvutano wa kijeshi kati ya pande hizo mbili.

  Msemaji wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric amesema, Bw. Guterres amepongeza maendeleo hayo yaliyopatikana katika mazungumzo ya ngazi ya juu kati ya pande hizo mbili tarehe 9 Januari.

  Bw. Gutteres pia amekaribisha uamuzi wa Korea Kaskazini kutuma ujumbe kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi itakayofanyika mwezi ujao nchini Korea Kusini, akitarajia kuwa jitihada hizo zitasaidia kurejesha mazungumzo ya dhati yatakayoleta amani ya kudumu na kutimiza lengo la kutokuwa na silaha za nyuklia kwenye Peninsula ya Korea.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako