• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ofisa wa UM aonya kuhusu hatari za kucheleweshwa kwa mchakato wa uchaguzi DRC

    (GMT+08:00) 2018-01-10 09:03:57

    Naibu katibu mkuu wa umoja wa mataifa anayeshughulikia ulinzi wa amani Bw. Jean Pierre Lacroix, amesema kuendelea kucheleweshwa kwa mchakato wa uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kunaweza kuchochea mivutano ya kisiasa na kuhatarisha hali ya usalama.

    Katika miezi ya hivi karibuni makundi yenye silaha yamekuwa yakifanya mashambulizi dhidi ya majeshi ya serikali, kusababisha hasara ya kudhibiti maeneo yenye raslimali. Amesema shambulizi la hivi karibuni ni lile lililofanywa na kundi la ADF na kusababisha vifo vya walinzi wa amani 15 kutoka Tanzania na wengine 44 kujeruhiwa

    Makubaliano ya kisiasa yalifikiwa mwaka 2016 na kumruhusu rais Joseph Kabila kuendelea kuwepo madarakani baada ya muda wake kumalizika, kwa sharti kuitisha uchaguzi mkuu mwaka jana. Lakini hilo halikutekelezwa kutokana na sababu za ugavi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako