• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Afrika Kusini kuunda tume ya uchunguzi kuhusu mafisadi kuwa na ushawishi serikalini

    (GMT+08:00) 2018-01-10 09:22:11

    Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ametangaza kuwa ameamua kuunda tume ya uchunguzi kuhusu mafisadi kuwa na ushawishi serikalini.

    Rais Zuma amesema, uamuzi huo umefikiwa kutokana na uchunguzi na hatua za marekebisho zilizopendekezwa na mlinzi wa mali za umma wa zamani Bw. Thuli Madonsela kuhusu tuhuma za mafisadi kuwa na ushawishi serikalini pamoja na uamuzi wa mahakama kuhusu suala hilo.

    Mahakama ya ngazi ya juu ya jimbo la Gauteng Kaskazini Desemba 14 mwaka jana ilimwamuru rais Zuma aunde kamati ya uchunguzi kuhusu mafisadi kuwa na ushawishi serikalini ndani ya siku 30. Mara baada ya kutolewa kwa uamuzi huo, rais Zuma alipinga uamuzi huo akisema uamuzi huo ulitolewa kwa msingi wa mashaka yasiyothibitika na ushahidi wa kijuujuu.

    Rais Zuma anatuhumiwa kushirikiana na familia ya Gupta ya India katika kupora mali za taifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako