• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa mawaziri barani Afrika wasisitiza haja ya kukabiliana na suala la uhamiaji kwa njia shirikishi

    (GMT+08:00) 2018-01-10 09:40:51

    Kwenye mkutano wa mawaziri kuhusu agenda ya Afrika juu ya suala la uhamiaji uliofanyika jana huko Rabat, Morocco, maofisa wa serikali za nchi za Afrika wamesisitiza haja ya kukabiliana na suala la uhamiaji kwa njia shirikishi.

    Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wa Morocco Bw. Nasser Bourita amesema, ajenda ya Afrika kuhusu suala la uhamiaji italifanya suala la uhamiaji liwe kichocheo cha maendeleo ya ushirikiano, nguzo ya ushirikiano wa kusini na kusini, na mwelekeo wa kuhimiza mshikamano.

    Waziri wa mahusiano ya kimataifa na ushirikiano wa Afrika Kusini Bibi Maite Nkoana-Mashahane, amesema kama suala la uhamiaji litashughulikiwa vizuri, litaleta fursa nyingi kwa Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako