• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rwanda kucheza na Algeria leo, kwa ajili ya kujiandaa na CHAN 2018

  (GMT+08:00) 2018-01-10 10:19:22

  Timu ya taifa ya soka ya Rwanda leo inashuka dimbani kucheza mechi ya kirafiki na Algeria kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (yaani CHAN) yatakayoanza januari 13 nchini Morocco.

  Mechi hiyo inafanyika katika uwanja wa Olimpiki el Menzah mjini Tunis, na itatoa tathmini halisi ya maandalizi ya kikosi cha kocha Antoine Hey kabla ya kuanza rasmi kwa mashindano.

  Rwanda tayari wamecheza mechi mbili za maandalizi, moja ikiwa ni dhidi ya Sudan ambayo ilidumu kwa dakika arobaini tu jumamosi iliyopita baada ya wachezaji kuzozana na nyingine iliyoisha kwa sare ya goli 1-1 dhidi ya Namibia siku ya jumapili.

  Timu hiyo inatarajiwa kuelekea Morocco kesho kwa ajili ya mashindano ambako iko kundi C paomja na timu za Libya, Nigeria na Equatorial Guinea.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako