• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Washindi wa medali za kimataifa waomba kusaidiwa katika maadalizi

  (GMT+08:00) 2018-01-10 10:20:17
  Wanaridha chipukizi kutoka nchini Rwanda, Salome Nyirarukundo na James Sugira amabo wote kwa pamoja walishinda medali ya fedha kila mmoja katika mashindano ya kimataifa yaliyomalizika Disemba 30 mjini Trier nchini Ujerumani, wameiomba jamii ikiwemo serikali kuwaunga mkono kwa hali na mali wanamichezo kila wanapojianda na mashindano ili wafanikiwe kuitetea vyema bendera ya Taifa.

  Naye mkurugenzi wa ufundi wa chama cha riadha cha Rwanda Jean Pierre Ndacyayisenga amabye aliambatana na wanariadha hao, alikiri kuwa maandalizi hafifu yalikuwa kikwazo kwa vijana hao kushinda medali za dhahabu katika mashindano yaliyojimuisha wanariadha 1600 kutoka nchi 27 duniani.

  Washindi wa medali za dhahabu katika mbio hizo za Ujerumani walikuwa Konstanze Klosterhalfen ujerumani kwa upande wa wanawake na Zouhair Talbi wa Morocco kwa upande wa wanaume.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako