• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kombe la ligi Uingereza: Manchester City yashinda nusu fainali ya kwanza

  (GMT+08:00) 2018-01-10 10:20:59
  Klabu ya Manchester city imeshinda mechi yake ya kwanza ya nusu fainali ya kombe la ligi nchini Uingereza kwa magoli 2-1 ilipocheza dhidi Bristol City katika uwanja wa Etihad.

  Goli la dakika za majeruhi lililofungwa na Sergio Aguero ndio liliinusuru kupata sare city, baada ya mechi hiyo kuonekana ngumu sana kutokana na uimara wa Bristol.

  Bristol ndio waliokuwa wa kwanza kupata goli katika dakika ya 44, ambalo Kevin De Bruyne alilisawazisha kunako dakika 55.

  Timu hizo zinarudiana Januari 23 ili kufuzu kwa fainali, na mshindi atakutana na mshindi katika mechi nyingine ya nusu fainali kati ya Chelsea na Arsenal.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako