• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uchumi wa China kuendelea kukua kwa pande zote katika miongo ijayo

  (GMT+08:00) 2018-01-10 18:24:15

  Makamu wa rais wa zamani na mchumi mkuu wa Benki ya Dunia Justin Lin Yifu amesema, China ina uwezo wa kudumisha ukuaji wa uchumi wa mwaka wa asilimia 6 mpaka itakapofika miaka ya 2030.

  Li amesema hayo alipokuwa akihutubia hafla ya "Makadirio: Uchumi wa China 2018" iliyoandaliwa na Kamati ya Taifa ya Uhusiano wa China na Marekani na Kituo cha Chuo Kikuu cha Peking cha Utafiti wa Uchumi iliyofanyika mjini New York, Marekani. Mchumi huyo amefafanua kuwa, njia ya kudumisha ukuaji wa uchuni ni kuboresha pato la jumla la uzalishaji nchini humo, na njia ya kufanya hivyo ni kuwa na uvumbuzi wa kiteknolojia na kuboresha sekta ya viwanda.

  Kwa miaka ijayo, mchumi huyo amekadiria kuwa China itaendelea kudumisha ukuaji wa kasi wa uchumi ikilinganishwa na nchi zilizoendelea.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako