• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uchumi wa Tanzania waendelea kuwa imara

  (GMT+08:00) 2018-01-10 19:42:46

  Serikali ya Tanzania imesema hali ya uchumi wa nchi hiyo inaendelea kuwa imara kwa kiasi cha kuridhisha taasisi mbalimbali za kimataifa. Kwa mwaka huu wa fedha, uchumi unatarajiwa kukua kwa asilimia 6.5 hadi 7.0 na kuifanya Tanzania kuendelea kuwa kati ya nchi tano bora za Afrika.

  Msemaji wa Serikali Hassan Abbasi amesema ripoti ya Shirika la Fedha Duniani (IMF), Benki ya Dunia (WB) na Taasisi ya Goldman Sachs ya Marekani zimetabiri kuwa wakati uchumi wa dunia utakua kwa wastani wa asilimia 3.0 hadi 4.0, ukuaji wa uchumi wa Tanzania unatajwa kuendelea kuwa kati ya nchi tano bora za Afrika ukitarajiwa kukua kwa asilimia 6.5 hadi 7.0 katika mwaka 2018.

  Aidha ameongeza kuwa moja ya ajenda kuu za Serikali ya Awamu ya Tano ni kujenga uchumi mpya wa viwanda, ambapo hadi kufikia mwaka jana viwanda 3,300 vilisajiliwa, Ujenzi na uzalishaji katika viwanda hivyo uko katika hatua mbalimbali. Amesema kati ya miradi hiyo iliyosajiliwa, viwanda vikubwa ni 652 na viwanda hivyo vyote vina jumla ya mtaji wa zaidi ya shilingi trilioni tano, utakaowekezwa nchini humo na vitaajiri watu 50,625 ambapo mwezi ujao Alisema, katika sekta ya nishati, Serikali inaendelea kutekeleza miradi 20 ya kuhakikisha nchi ina umeme wa uhakika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako