• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya na Tanzania miongoni mwa nchi bora kutalii 2018

  (GMT+08:00) 2018-01-10 19:43:29

  Shirika la utalii la kimataifa The Travel Corporation (TTC) limeorodhesha Kenya na Tanzania kuwa vituo vya nafasi ya kwanza duniani vya kutembelewa mwaka 2018 .

  Shirika hilo limetaja hasa safari ya 11 kuanzia mji mkuu wa Kenya Nairobi, hadi kwenye hifadhi maarufu ya masai mara na ile ya Serengeti nchini Tanzania kama miongoni mwa maeneo 10 ya kwanza ya kutalii mwaka huu.

  Mkurungezi wa TTC Brett Tollman aidha amesema safari hiyo inajumuisha kambi za hema, kuendesha gari ndani ya hifadhi ya wanyama na hatimaye kukamilisha kisiwani Zanzibar.

  Maeneo mengine yaliotajwa bora ya kutalii ni pamoja na Norway, India's golden triangle, London na Berlin .

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako