• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Magufuli asema bado kuna matatizo bandarini

  (GMT+08:00) 2018-01-10 19:43:52

  Rais Magufuli aRais John Pombe Magufuli wa Tanzania amesema amebaini matatizo mengi katika bandari ya Dar es Salaam, ikiwemo kuwepo kwa makontena mengine yenye mabaki ya mchanga wenye madini ya dhahabu (makinikia).

  Aidha Magufuli amempa waziri wa Madini Bi. Angela Kairuki na Waziri wa Kilimo na Chakula Charles Tizeba siku tano kusimamia utekelezaji wa majukumu yaliyo chini ya wizara zao, vinginevyo watalazimika kuachia nafasi zao. Rais alisema hayo mjini Dar es Salaam baada ya kumwapisha Naibu Waziri wa Madini Dotto Biteko aliyemteua kushika wadhifa huo na kufanya wizara hiyo kuwa na Naibu Waziri wawili.

  Akizungumzia matatizo bandarini, Rais Magufuli amesema alipotembelea bandari hiyo Septemba mwaka jana, aliunda timu ya siri ambayo ilihusisha wajumbe mbalimbali wakiwemo kutoka Jeshi la Ulinzi wa Wananchi (JWTZ), Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ili kuichunguza kwa kina zaidi bandari hiyo. Rais Magufuli aliwataka viongozi wote kila, mmoja kughulikia eneo lake kwa hali ya juu na kwamba wasisubiri kuoneshwa uozo unaoendelea ndani ya taasisi walizopo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako