• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • IOC kuamua ushiriki wa Korea Kaskazini kwenye michezo ya Olimpiki ya PyeongChang

  (GMT+08:00) 2018-01-11 08:51:17

  Kamati ya Olimpiki ya kimataifa IOC imesema itaitisha mkutano wa pande nne ili kufanya uamuzi kuhusu ushiriki wa Korea Kaskazini kwenye michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya mwaka huu itakayofanyika mwezi ujao mjini PyeongChang, Korea kusini. Mkutano huo utafanya maamuzi kuhusu idadi na majina ya wachezaji na maofisa kutoka Korea Kaskazini, kwa kuwa muda wa uandikishaji umekwisha. Kwenye taarifa iliyotolewa na IOC, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bw. Thomas Bach amekaribisha maombi ya pamoja yaliyotolewa na Korea kusini na Korea Kaskazini, na kuyataja kuwa ni hatua kubwa iliyopigwa na pande hizo mbili kwa moyo wa Olimpiki na makubaliano ya kusitisha vita katika kipindi cha michezo ya Olimpiki yaliyopitishwa kwenye Baraza kuu la Umoja wa Mataifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako