• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa mataifa wasema uchaguzi ni muhimu kwa utulivu wa Libya

    (GMT+08:00) 2018-01-11 09:27:05

    Naibu katibu mkuu wa umoja wa mataifa anayeshughulikia mambo ya kisiasa Bw. Jeffrey Feltman, amesema kufanya uchaguzi ndio njia pekee ya kuleta utulivu nchini Libya.

    Bw. Feltman amesema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari baada ya kukutana na waziri mkuu wa Libya Bw Fayez Serraj mjini Tripoli, ambako walibadilishana maoni kuhusu maendeleo ya kisiasa nchini Libya na umuhimu wa kutoa sheria mpya ya uchaguzi na sheria mpya ya kura za maoni ya katiba.

    Bw. Feltman amesema katibu mkuu wa umoja wa mataifa amedhamiria kuwaunga mkono watu wa Libya wakati wanaendelea kufanya kazi ya kuandaa kura za maoni kuhusu katiba, kufanya uchaguzi na masikilizano ya kikanda na kitaifa. Amesema kuna dalili zenye nguvu zinazoonyesha kuwa vyama vya siasa na viongozi wa Libya wanaunga mkono uchaguzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako