• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kombe la Mapinduzi: Azam FC kucheza na URA jumamosi

  (GMT+08:00) 2018-01-11 09:28:01

  Mabingwa wa kombe la mapinduzi Azam FC wamefanikiwa kufuzu fainali ya mashindano hayo msimu huu baada ya ushindi wa goli 1-0 waliopata jana kwenye mechi ya nusu fainali dhidi ya Singida United mjini Zanzibar.

  Goli la ushindi kwa Azam lilipatikana kupitia Shaaban Idd kunako dakika ya 78 kwa shuti lililomshinda kipa wa Singida United Peter Manyika.

  Kwa ushindi huo Azam FC watakutana na URA kwenye mechi ya fainali itakayopigwa jumamosi Januari 13.

  URA iliingia fainali baada ya kuwatupa nje Yanga ya Dar es Salaam kwa magoli ya penati ya 5-4 baada ya mechi yao ya nusu fainali kuisha kwa matokeo ya 0-0 katika dakika 90 za kawaida.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako