• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kombe la Dunia 2019 China: Wachezaji 17 wateuliwa kuunda timu ya Rwanda

  (GMT+08:00) 2018-01-11 09:28:26

  Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Rwanda ya mchezo wa mpira wa kikapu, Moise Mutokambali, amatangaza majina ya awali 17 ya wachezaji 17 watakaounda kikosi kitakachojiandaa na mzunguko wa kwanza wa mshindano ya kufuzu kombe la dunia mwaka 2019.

  Timu hiyo imeanza rasmi kambi ya mazoezi jana jumatano kwenye uwanja wa ndani wa Amahoro na ikitarajiwa kufanya mazoezi mara mbili kwa wiki.

  Rwanda iko kundi B la mechi za kufuzu, ikiwa na timu za Mali, Nigeria, Uganda na mechi za timu hizo zikitarajiwa kufanyika kati ya Februari 23-25 mjini Bamako.

  Kombe la dunia la mpira wa kikapu litafanyika mwezi Agosti hadi Septemba mwaka 2019 nchini China.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako