• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kombe la Ligi Uingereza: Chelsea na Arsenal zatoka sare nusu fainali

  (GMT+08:00) 2018-01-11 09:29:42
  Licha ya klabu ya Chelsea kuongoza kwa muda mrefu zaidi kuliko wapinzani kwenye mechi ya jana ya nusu fainali ya kwanza ya kombe la ligi nchini Uingereza, imeshindwa kuondoka na ushindi ilipocheza dhidi ya Arsenal katika uwanja wa Stamford Bridge.

  Kocha mkuu wa Chelsea, Antonio Konte, amesema sare hiyo inawapa changamoto kuelekea mechi ya marudio watakapokuwa ugenini kwani watalazimika kucheza kama fainali ili kusawazisha makosa ya mechi ya jana.

  Timu hzio zinatarajiwa kurudiana Januari 23, na Chelsea wanasaka kwa udi na uvumba kombe hilo ambalo hawajakuwa na bahati nalo, huku Arsenal nao wakiamini kuwa ndilo tumaini pekee lililobaki, kutokana na nafasi kuwa finyu katika ligi kuu, hukuwakiwa wameondolewa kwenye mashindano ya kombe la FA.

  Mshindi wa mechi ya nusu fainali hii atakutana na mshindi wa nusu fainali nyingine kati ya Manchester City na Bristol City.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako