• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wabunge wa Afrika Kusini waanza kujadili sheria za kumwondoa rais madarakani

    (GMT+08:00) 2018-01-11 09:35:35

    Kamati ya bunge la Afrika Kusini ilikutana jana kujadili kanuni za kumwondoa madarakani rais, wakati kuna uvumi kuwa rais Jacob Zuma wa nchi hiyo atajiuzulu.

    Mwenyekiti wa kamati ya ukaguzi wa sheria Bw. Richard Mdakane amesema, hii inahusiana na kifungu cha 89 cha Katiba ya nchi ambacho kinashughulikia kuondolewa madarakani kwa rais kutokana na ukiukaji wa katiba au sheria, uongozi mbaya, au kushindwa kutelekeza majukumu ya kiofisi.

    Mjadala huo ulifanyika kufuatia uamuzi uliotolewa mwezi wa Desemba na mahakama ya kikatiba, iliyoliamuru bunge la taifa kutunga kanuni za kumwondoa rais bila kuchelewesha, ili kuanzisha mchakato wa kumwondoa madarakani rais Zuma.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako