• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • WHO yatoa chanjo ya kipindupindu kwa watu milioni 1 nchini Zambia

  (GMT+08:00) 2018-01-11 09:38:17

  Shirika la Afya Duniani WHO limesema linaiunga mkono Zambia kuanzisha kampeni ya kutoa chanjo ya kipindupindu kwa wananchi wake milioni moja.

  Kampeni hiyo imeanza jana kwa wakazi wa Lusaka, ambapo dozi milioni mbili za chanjo hiyo zimefikishwa nchini Zambia mwezi huu, kiasi ambacho kinawatosha watu milioni moja. Idara ya afya ya Zambia imesema chanjo hiyo itatolewa kwanza kwa wale wanaoihitaji zaidi.

  Kipindupindu ni ugonjwa wenye hatari kubwa ya kusababisha vifo ndani ya muda mfupi kama hakuna matibabu ya haraka. Tangu mwezi Oktoba mwaka jana, idadi ya wagonjwa wa kipindupindu nchini Zambia iliripotiwa kufikia 2,672, na 2,558 kati yao walitoka mjini Lusaka.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako