• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Baraza la usalama la Ethiopia lasema hali ya usalama imeboreshwa

  (GMT+08:00) 2018-01-11 15:03:06

  Baraza la usalama la taifa la Ethiopia ENSC limesema hali ya usalama nchini Ethiopia imeboreshwa katika siku 45 zilizopita.

  Waziri wa ulinzi wa Ethiopia na mratibu wa baraza hilo Bw. Siraj Fegessa amesema hatua walizochukua kuzuia hali ya barabara kuzingirwa na waandamanaji na mikutano haramu, zimefanikiwa. Pia amesema silaha mbalimbali zilikamatwa zikiwa njiani kupelekwa Addis Ababa.

  Mwaka 2016 vurugu katika majimbo makubwa ya Ethiopia ziliilazimu serikali kutekeleza sheria za kijeshi, na baada ya mwaka 2017 hali kutulia serikali iliondoa sheria hizo, Hata hivyo kuanzia mwezi Septemba serikali ya Ethiopia imekuwa na hofu kuhusu kuongezeka kwa dalili za vuguru katika majimbo mawili ya Oromia na Amhara.

  Waoromo na waamhara wanaochukua asilimia 33 na 27 ya Waethiopia, wanawashutumu Watigray ambao ni asilimia sita wa Waethiopia, kudhibiti siasa na uchumi wa nchi hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako