• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AMISOM yatoa mafunzo kwa polisi wa Somlia kuhusu alama za vidole

    (GMT+08:00) 2018-01-11 15:03:28

    Tume maalumu ya Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM imeanza mafunzo ya wiki mbili kwa polisi wa Somalia kuhusu utambuzi wa alama za vidole uchunguzi wa matukio ya jinai.

    Mratibu wa polisi jimbo la kusini magharibi Bw. Tresphord Kasale amesema washiriki watapewa mafunzo ya kuchukua, kuhifadhi na kuzifanyia kumbukumbu alama za vidole kwa ajili ya kushughulikia kesi za jinai.

    Ameongeza kwamba mafunzo hayo yatafanyika huko Baidoa, kuwalenga maofisa kutoka idara ya upelelezi wa makosa ya jinai ya kusini magharibi (CID).

    Msaidizi wa waziri wa usalama wa jimbo la kusini magharibi wa nchi hiyo Bw. Abdirizak Aden Abdi amesema mafunzo hayo ni muhimu katika kuendeleza uchunguzi wa jinai na kuwatambua washukiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako