• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lapongeza maingiliano kati ya nchi mbili za Korea

  (GMT+08:00) 2018-01-11 18:18:45

  Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepongeza mawasiliano ya hivi karibuni katika Peninsula ya Korea, lakini limesisitiza kudumisha vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini.

  Mwenyekiti wa zamu wa baraza hilo ambaye pia ni balozi wa Kazakhstan kwenye Umoja wa Mataifa Kairat Umarov amesema, wajumbe wa baraza hilo wamesema majadiliano kama hayo kati ya nchi mbili za Korea yanaweza kufungua fursa ya kujiamini na kujenga uaminifu katika Peninsula ya Korea, kupunguza mvutano, na yanaweza kusaidia katika kutimiza kutokuwa na silaha za nyuklia katika peninsula hiyo.

  Jumanne wiki hii Korea Kusini na Korea Kaskazini zilianza majadiliano ya ngazi ya juu, ikiwa ni ya kwanza kufanyika katika miaka miwili, kwenye kijiji cha Panmunjom, ambacho kipo katikati ya eneo la mpaka wa nchi hizo mbili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako