• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Beijing kupunguza msongamano barabarani

  (GMT+08:00) 2018-01-11 18:26:34

  Beijing itachukua hatua kupunguza msongamano barabarani. Hayo yamesemwa leo na msemaji wa kamati ya mawasiliano ya barabara ya mji wa Beijing Bw. Rong Jun. Ameeleza kuwa hatua hizo ni pamoja na kuharakisha ujenzi wa treni zinazopita chini ya ardhi, kuboresha mtandao wa mabasi, na kurekebisha njia za kupita kwa baiskeli, ili kuongeza kiasi cha safari zisizoleta uchafuzi wa mazingira na kuwa asilimia 73.

  Bw. Rong Jun amesema, mwaka jana safari zisizoleta uchafuzi wa mazingira kwenye sehemu za katikati za Beijing zilichukua asilimia 72, na kiwango cha msongamano barabarani kilikuwa 5.6, ambacho ni cha ngazi ya chini. Mwaka huu, Beijing itachukua hatua kadhaa ili kuboresha zaidi hali ya mawasiliano barabarani. Bw. Rong anasema,

  "Tutaendelea kuharakisha ujenzi wa treni zinazopita chini ya ardhi, na urefu wa njia za treni hizo utaongezeka na kuwa zaidi ya kilomita 632. Pia tutaendelea na juhudi za kuboresha mtandao wa mabasi, na kurahisisha mahitaji ya kubadilisha vyombo vya usafiri. Aidha, tutarekebisha njia zinazopitabaiskeli kwa urefu wa zaidi ya kilomita 900, na kuhakikisha haki ya kupita barabarani kwa vyombo vya usafiri vinavyoenda polepole, pia kuongeza kiasi cha safari zisizoleta uchafuzi wa mazingira na kuwa asilimia 73 kutoka 72."

  Kuanzia mwaka 2003 hadi hivi sasa, serikali ya Beijing imemaliza miradi zaidi ya 2,200 ya kupunguza msongamano barabarani, haswa kwa njia ya kuboresha njia panda, kurekebisha sehemu za kutoka na kuingia barabara kuu, kujenga barabara za kupita kwa mabasi tu na kuongeza vituo vyake. Miradi hiyo imetoa mchango mkubwa katika kupunguza msongamano kwenye baadhi ya sehemu. Bw. Rong amesema kazi muhimu zaidi ya mwaka huu ni kukamilisha mpango na sehemu za kuegesha magari na utekelezaji wake ndani ya barabara ya mzunguko wa pili. Anasema,

  "Pia tutaongeza ukaguzi dhidi ya vitendo vya kuegesha magari ovyo. Tutahimiza uwekaji wa utaratibu wa kuegesha magari, na kutekeleza mpango na sera husika."

  Baiskeli za kuchangia zimesaidia kupunguza msongamano barabarani. Wakati huo huo, vitendo vya kuziweka ovyo vimeleta athari mbaya. Naibu mkuu wa idara ya uchukuzi ya kamati ya mawasiliano ya barabara ya mji wa Beijing Bw. Yang Yuliang amesema, serikali ya Beijing itatatua suala hilo kwa njia ya sheria. Anasema,

  "Mwaka huu tutasukuma mbele kazi za utungaji wa sheria kuhusu vyombo vya usafiri visivyo vya kimota, ili kudhihirisha majukumu ya serikali na mashirika, na kutatua suala la baiskeli za kuchangia."

  Mbali na hayo, Beijing itaendelea kuweka kipaumbele katika safari zisizoleta uchafuzi wa mazingira. Na inakadiriwa kuwa mwaka huu treni tatu mpya zinazopita chini ya ardhi zitazinduliwa na kuanza kuwahudumia wakazi wa Beijing.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako