• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uamuzi wa Iran wa kutekeleza makubaliano ya suala la nyuklia wategemea kitendo cha Marekani

    (GMT+08:00) 2018-01-11 19:35:55

    Waziri wa mambo ya nje wa Iran Bw. Javad Zarif amesema, Iran itaendelea kutekeleza ahadi zake zote katika makubaliano ya suala la nyuklia la nchi hiyo yaliyosainiwa mwaka 2015, kama Marekani nayo itafanya hivyo pia.

    Bw. Zarif amesema, pande zote zimekubaliana kuwa ni muhimu zaidi kutekeleza kikamilifu makubaliano hayo, na pia Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki IAEA limethibitisha utekelezaji wa Iran katika makubaliano hayo.

    Habari zinasema, Bw. Zarif anatarajia kuzungumza na viongozi wa Russia, Umoja wa Ulaya, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani kuhusu suala hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako