• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya:Bei ya sukari yashuka

  (GMT+08:00) 2018-01-11 19:42:57

  Bei ya sukari imeshuka kwa asilimia 27 katika kwa miezi miwili sasa kufuatia ongezeko la bidhaa hiyo kutoka nje.

  Takwimu kutoka kwa idara ya kudhibiti sukari nchini inaonyesha kwamba gunia moja la sukari la kilo 50 linauzwa shilingi elfu 4 kutoka 5500 mwezi Agosti mwaka jana.

  Bei ya reja reja ya sukari aidha imeshuka kutoka shilingi 400 kwa kilo 2 hadi 250.

  Alfred Busolo mkurugenzi mkuu wa halmashauri ya kilimo nchini Kenya amesema kuimarika kwa uzalishaji wa bidhaa pia kumechangia kwa bei hiyo mpya.

  Kutoka mwezi Agosti sukari iliongezeka kwa mita tani elfu 6 kutoka elfu 3 .

  Wafanyibiashara waliagiza jumla ya mita tani laki tatu kuanzia mwezi Agosti mwaka jana.

  Mwaka jana ukame uliathiri pakubwa kwa uzalishaji wa sukari na kuchangia kupanda kwa bei ya sukari kwa zaidi ya asilimia 100.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako