• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda:wafanyibiashara wa Uganda walalamikia marufuku ya safari za usiku Kenya

  (GMT+08:00) 2018-01-11 19:43:41

  Wafanyibiashara wa Uganda wamelalamikia kuathirika kwa biashara zao kutokana na marufuku ya safari za usiku za magari ya umma .

  Mwenyekiti wa muungano wa wafanyibiashara wa Uganda Everest Kayondo amesema marufuku hayo yameongeza mda wa uchukuzi wa bidhaa zao hivyo kuchangia kupanda kwa gharama na bei.

  Safari ya siku tatu kutoka Uganda hadi baadhi ya sehemu nchini Kenya sasa zimefikia siku 6.

  Wafanyibiashara hao sasa wameitisha kikao na wizara ya biashara ya Kenya kujadiliana kuhusiana na tarifu za kuondoa vikwazo mipakani.

  Marufuku hayo yamechangia msongamano mkubwa wa mabai ya umma mpakani yanayowasili kwa wakati mmoja na kuhitaji kuhudumiwa.

  Kenya ilipiga marufu mabasi ya uchukuzi wa umma kutokana na ajali nyingi za mara kwa mara.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako