China imeukaribisha mpango wa Umoja wa Ulaya kuunganisha pendekezo la "Ukanda mmoja Njia moja" la China, na mpango wake wa mafungamano ya mabara ya Asia na Ulaya. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China Bw. Lu Kang amesema China iko tayari kushirikiana na Umoja wa Ulaya kwenye ushirikiano wa kunufaishana, kuhimiza ustawi na utulivu katika mabara ya Asia na Ulaya, na kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |