• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mwenyekiti mpya wa chama cha ANC ataka migogoro ndani ya chama hicho ikomeshwe

  (GMT+08:00) 2018-01-12 08:54:28

  Mwenyekiti wa chama tawala cha Afrika Kusini ANC Bw. Cyril Ramaphosa ametoa mwito wa kumaliza mivutano ndani ya chama cha ANC.

  Akiongea mjini East London, katika jimbo la Cape Mashariki kabla ya maadhimisho ya miaka 106 ya ANC, Bw Ramaphosa amewataka viongozi wa chama hicho kuungana na kuongea kwa sauti moja. Amesema uchaguzi sasa umeisha na mshindi ni chama cha ANC.

  Bw. Ramaphosa ametoa kauli hiyo wakati mvutano kati ya wanachama wa ANC kuhusu hatma ya Rais Jacob Zuma ukiendelea. Kuna wanaotaka Rais Zuma aondolewe madarakani na wengine wakipinga uamuzi huo. Wakati huo huo bunge linaendelea kujadili kanuni na taratibu za kumwondoa madarakani Rais Zuma.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako