• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Vyama vya Ethiopia vyajadili sheria ya kupambana na ugaidi

  (GMT+08:00) 2018-01-12 09:12:30

  Vyama vya Ethiopia ambavyo vinafanya majadiliano kuhusu sheria ya kupambana na ugaidi, vimekubali kusikiliza mashauri ya chama tawala juu ya pendekezo lao kuhusu sheria hiyo.

  Vyama vya upinzani vimewasilisha pendekezo la kurekebisha sheria hiyo, vikisema sheria hiyo inaenda kinyume na katiba na maazimio ya haki za binadamu ya kimataifa. Aidha, vimetoa mwito wa kuhimiza mchakato wa kuwaachia huru baadhi ya wanasiasa waliowekwa kizuizini.

  Waziri mkuu wa Ethiopia Bw Hailemariam Desalegn pamoja na viongozi wa vyama vinne wanachama wa chama tawala cha EPRDF, wametangaza kuwa wanasiasa waliowekwa kizuizini watafutiwa mashtaka na kuachiwa huru. Bw Desalegn amesema hatua hiyo itahimiza umoja, masikilizano na mazungumzo, na kwamba serikali ya Ethiopia itafunga gereza la mahabusu la Maekelawi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako