• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Zimbabwe kufanya ziara nchini Namibia

  (GMT+08:00) 2018-01-12 09:19:49

  Ikulu ya Namibia imesema rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe atafanya ziara nchini Namibia Januari 15. Taarifa iliyotolewa na Ikulu hiyo inasema, akiwa ziarani rais Mnangagwa atafanya mazungumzo na mwenzake wa Namibia Bw Hage Geingob.

  Taarifa pia imesema, ziara hiyo itafanyika kwa kufuata maslahi ya baadaye yatakayoimarisha uhusiano kati ya pande mbili, na kufikiria uwezekano wa maeneo mapya ya ushirikiano.

  Tangu aingie madarakani Rais Mnangagwa ametembelea Afrika Kusini, na leo anatarajiwa kutembelea Angola.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako